Maudhui Ya Ukatili Wa Kingono Kwa Mtoto (Child Sexual Abuse/ExploitationMaterials)

Maudhui Ya Ukatili Wa Kingono Kwa Mtoto (Child Sexual Abuse/ExploitationMaterials)

Maendeleo na ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano nchini na duniani kwa ujumla, imesababisha kuwepo kwa matumizi ya mtandao na vifaa vya kielekroniki yaliyo sahihi na yasiyo sahihi.

Kutokana na jamii kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu matumizi sahihi na salama ya mtandao na vifaa vya kielektroniki, kumekuwepo na usambazwaji wa picha mnato, video, maandishi, miziki, na kazi nyingine za sanaa zenye maudhui ya kingono.

Aidha, maudhui hayo yamekuwa na athari kwa watoto na jamii kwa ujumla zikiwemo;

Msongo wa mawazo unaoweza kusababisha kujiua, wakati mtoto anaona vitisho au maudhui ya kumdhalilisha na hivyo kudhani hana msaada na badala yake anafikia uamuzi wa kujiua.

 

Mtoto anaweza kujikuta akishiriki ngono katika umri mdogo, ikiwa ataona au kuoneshwa maudhui ya kingono au yenye mwelekeo wa kingono inamshawishi mtoto kujaribu na kushiriki ngono.

Inachochea kushiriki ngono ya jinsia moja na kinyume na maumbile, pale ambapo mtoto anaona kwa mara ya kwanza maudhui ya ngono kwa watu wa jinsia moja, husababisha aone kwamba ni jambo la kawaida. Hali hii humfanya akue akijua ngono ya jinsia moja ni sahihi.

Kuhusishwa kwenye biashara ya ngono, mtoto anaweza  kurubuniwa kwa kushiriki katika kupiga picha za utupu au kufanya vitendo vinavyoashiria ngono kwa minajili ya kulipwa ujira.

Watoto kutumikishwa katika masuala ya ngono kwa kupigwa picha au kuchukuliwa video na kutishwa ili wasitoe taarifa kwa wazazi au walezi. Kutokana na vitisho watoto huendelea na shughuli hizo bila kutoa taarifa au kuomba msaada akiamini anajilinda na anawalinda watu wake wa karibu.

Kutokuwa na uelewa wa sheria, kanuni na sera zinazomlinda mtoto kama vile Sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 inayolinda haki za watoto, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 Kifungu cha 13 inayokataza kuweka au kuwahusisha watoto na Maudhui ya Kingono, na Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008.

UJUMBE


Kwa Watoto

 1. Mtoto epuka kutuma na kuhifadhi picha au video zenye maudhui ya kingono. Kwa mujibu wa sheria ya Makosa ya Mtandaoni ya Mwaka 2015 (14) ni kosa la jinai.

 

 1. Mtoto toa taarifa kwa mzazi/mlezi, mwalimu, kiongozi yeyote au piga simu namba 116 iwapo mtu atakuomba picha yako mtandaoni.

 

 • Epuka kutumia muda mrefu katika mtandao.

 

 1. Epuka kutoa taarifa zako mwenyewe mtandaoni

 

 1. Epuka kukubali urafiki na watu usiowafahamu mtandaoni.

 

Kwa Wazazi/Walezi

 1. Mzazi epuka kutoa taarifa muhimu za mtoto wako mtandaoni.

 

 1. Mzazi/mlezi zungumza na mtoto/watoto kuhusu matumizi sahihi ya mtandao.

 

 • Watoto watumie simu na vifaa vya mawasiliano chini ya uangalizi wa wazazi au walezi na vifaa hivyo viwekwe nywila.

 

 1. Epuka kutuma na kuhifadhi picha au video zenye maudhui ya kingono. Kwa mujibu wa sheria ya Makosa ya Mtandaoni ya Mwaka 2015 (14) ni kosa la jinai na adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka saba au faini isiyopungua Milioni 20.

 

Kwa Wadau/Jamii

 1. Mamlaka zitoe elimu kwa jamii kuhusu Sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 inayolinda haki za watoto, Sheria ya Makosa ya Mtandao ya mwaka 2015 inayokataza kuweka au kuwahusisha watoto na Maudhui ya Kingono, na Sera ya Maendeleo ya Mtoto ya mwaka 2008.

 

 1. Wadau na jamii washiriki kwenye masuala yanayouhusu usalama wa watoto katika mitandao.

 

 • Shule zitekeleze miongozo kuhusu matumizi ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

 

 1. Jamii izingatie maadili na malezi ya kitanzania, licha ya kuwepo kwa utandawazi.

 

 

Welcome to official site of Safer Internet Tanzania, a home of safer internet day, hosted and managed by Computing and Information Association.

 

Wasiliana Nasi

 •  Plot No 2AE 20, Nyerere Road, Opposite Quality Motors.
 • Phone 1 0756 348  364
  Phone 2 : 0758 707 370