Maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni 2019

Maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni 2019

Mwaka 2019, siku ya usalama mtandaoni iliadhimishwa kwa matukio mawili, kwanza ni uzinduzi wa tovuti   na kujenga uelewa kwa wanafunzi wa shule mbili za Dar es salaam ambazo ni shule ya sekondari Kambangwa na shule ya msingi Kibangu.

Siku ya tarehe 5, mwezi februari  2019, siku ya usalama mtandaoni ndiyo siku ambyo tovuti  hii safer internet Tanzania www.saferinternet.or.tz  iliwekwa mtandaoni.

Ambayo ni website mahususi kwa maswala yanahusu usalama mtandao kwa vijana na watoto.

Mafunzo Shule ya Msingi Kibangu

Siku ya tarehe 14 mwezi  februari , wanafunzi  31 wenye umri wa miaka kuanzia 10-12 walipewa mafunzo juu ya matumizi bora na salama ya mtandao ambapo mafunzo yalilenga hasa kuhusu ridhaa kwenye ulimwengu wa matandao yani ‘consent on virtual world’

Mambo mengi yalidaliliwa na wanafunzi kupata fursa kuelezea namna wanayopaswa kuomba ridhaa ana kuombwa ridhaa kwenye vitu au mambo mbalimbali kwenye ulimwengu wa mtandao.

Kwenye vikundi vya wanafauzi 3-4 wanafunzi walipata fursa ya kujibu maswali /changamoto mabli mbali zinazoohusu ridhaa mtandaoni  na kisha kila kikundi kupata fursa ya kuwasilisha majibu yao mbele ya wenzao.

Mafunzo Shule ya Sekondari Kambangwa

Siku ya tarehe 14 mwezi februari, wanafunzi 52  wenye umri  wa kuanzia miaka 14 -18 walipewa mafunzo juu ya matumizi bora na salama ya mtandao ambapo mafunzo yalilenga ni namna bora ya kutawala maisha  ya mtandaoni usasani kwenye maswala yanayohusu taarifa binafsi.

Kwenye vikundi vya wanafunzi 5-7 wanafunzi walipata fursa ya kujadili na kuelezae nini hasa wameweza kujifunza na kipi watafanya ili kufanya mtandao uwe bora na salama.

 

Ripoti ya tukio zima [English]

Date

05 February 2019

Tags

2019