Maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni 2018

Maadhimisho ya Siku ya Usalama Mtandaoni 2018

Kwa mara ya pili , Siku ya Usalama Mtandaoni iliazimishishwa kwa kuitembelea shule ya msingi ya Kibangu English Medium iliyopo Kibangu Dar es salaam ambapo wanafunzi wa darasa la sita na la saba wapatao 49 wenye umri kati ya miaka 11-14 walisherekea siku hiyo kwa kupewa elimu juu ya matumizi bora na salama ya mtandao.

Wakiwa kwenye kikundi vya wanafunzi sita (6), wanafunzi walijadili na kujibu maswali matatu, wataje mitandao mitatu ya kijamii wanayotumia, wanatumia mitandao hiyo kufanya nini na wanajisikiaje kutumia mitandao hiyo.

Kila kikundi kilichagua mtu mmoja wa kuwasilisha maoni/majibu ya kikundi kwa watu wote.

Hizi ni baadhi ya picha za tukio zima.

Ripoti ya tukio zima [English]

Date

06 February 2018

Tags

2018